Wakati ni Huu Sasa: Wanaharakati wa Vijijini na Mijini Wako Tayari Kubadili Maisha ya Wanawake

Tamko la Phumzile Mlambo-Ngcuka,Wakati ni Huu Sasa: Wanaharakati wa Vijijini na Mijini Wako
Tayari Kubadili Maisha ya Wanawake

Msaidizi Mwandamizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa yaani UN Under-Secretary-
General na Mkurugenzi Mtendaji, Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshughulikia Maswala ya
Wanawake, tamko kwa ajili ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake mwaka 2018
Mada ya mwaka huu inavutia maisha ya kusisimua ya wanaharakati wanawake ambao shauku
na kujitolea kwao vilitwaa haki za wanawake katika vizazi na vizazi, kwa ufanisi juhudi zao
zikaleta mabadiliko.

Tunasheherekea harakati isiyokuwa ya kawaida ya kidunia ya haki za
wanawake, usawa, usalama na haki, kutambua kazi isiyokwisha ya wanaharakati ambao
wamekuwa wakishinikiza vuguvugu hili la kidunia kwa ajili ya usawa wa kijinsia.
Tunachoshuhudia leo ni mkusanyiko mkubwa wa nguvu miongoni mwa wanawake duniani
kote, wakithibitisha nguvu ya sauti moja, wakitoa wito kwa ajili ya fursa na uwajibikaji,
wakichochea kasi ya mitandao ya umma na ushirikiano mpana na uongozi wa kiserikali. Hizi
harakati zinakua kutokana na kazi ya wanaharakati wa vizazi anuwai – kuanzia Hayati Kiongozi
Mtetezi wa Nadharia ya Haki na Usawa wa Wanawake Asma Jahangir wa Pakistan, hadi kizazi
kipya chenye nguvu kinachowasilishwa na wanawake vijana mathalani Jaha Dukureh wa
Gambia, Balozi wa Umoja wa Mataifa wa Ukarimu kwa Wanawake wa Umoja wa Mataifa kwa
ajili ya Afrika ili kukomesha ukeketaji wa wanawake na ndoa za utotoni.
Jamii zenye afya zina mchanganyiko mkubwa wa sauti na wenye kutoa ushawishi kuhusu
taratibu za vyombo vya dola kudhibitiana ili kuzuia matumizi mabaya ya madaraka, mlolongo
tofauti wa uzoefu na mitazamo, na mjadala unaotoa mwongozo katika kuchukua maamuzi.
Mahali ambapo sauti ni ghaibu, kuna pengo muhimu katika mfumo wa kijamii. Pindi sauti hizo
nyamavu zinapohesabiwa kwa mamilioni, tunatambua kwamba kuna jambo lisilokuwa kuwa
sawa katika ulimwengu wetu. Hali kadhalika, tunapoona na kusikia sauti hizo nyamavu
zinapoongezeka na kupaza sauti ya juu ya ushiriakiano, tunahisi nguvu ya jambo fulani lenye
haki.
Tunawapongeza sana wale wote waliozungumza kwa ujasiri kwa ajili ya upatikanaji wa usawa
mathalani wale waliopo katika vuguvugu la #MeToo movement, wale ambao miezi ya hivi
karibuni waliweza kupaza sauti zao kupitia mitandao ya kijamii katika nchi zaidi ya 85 ili
kuwatangaza adharani wale wanaowakandamiza wanyonge na kuonyesha jinsi gani pindi
wanawake wanaposaidiana, harakati hizi zinasaidia kushinda unyanyapaa na kuhakikisha
kwamba hadithi zao zinaaminika. Tunawashukuru sana wanawake waliozungumza katika
Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ambapo ushuhuda wao uliwawajibisha waliofanya vitendo vya
ubakaji kama silaha ya kivita. Tunasheherekea na kutambua wale waliotetea marekebisho ya
kisheria katika nchi kama Tunisia, ili kusitisha vipengele vinavyoruhusu wahalifu wa ubakaji
kuepuka kufunguliwa mashtaka ikiwa watawaoa wahanga wa uhalifu wao. Tunatambua jitihada
za wale wote waliofanya maandamano mitaani nchini India ili kukataa mauaji na vitendo vya
ubakaji kwa watoto vijana, na kugeuza maandamano hayo kuwa harakati kabambe
zinazoshirikisha jamii nzima. Tunawaheshimu viongozi wa asili ambao walisimama kidete ili
kulinda haki za kijadi na kulinda ardhi na mila na desturi zao, na watetezi wa haki za binadamu
ambao hata walipoteza uhai wao kwa ajili ya kutetea itikadi zao.
Vuguvugu la utaratibu wa vyombo vya dola kudhibitiana ili kuzuia matumizi mabaya ya
madaraka linatakiwa kuendelea na kuongeza hali ya uwanuwai na idadi ya watu
wanaoshughulika na maswala ya usawa wa jinsia, kwa kuwashirikisha watu binafsi na
makundi—mathalani wanaume na wavulana, vijana na mashirika ya kidini—ili kuunga mkono
na kushadidisha agenda hii, ili wanaume vijana na wavulana waweze kujifunza kuwathamini na
kuwaheshimu wanawake na wasichana ili wanaume waweze kubadili tabia zao. Harakati ya leo
inahitaji kubadili mwelekeo wa jinsi tunavyowasikiliza wanawake na namna tunavyowaangalia,
kwa kutambua nguvu ya kasumba iliyokubalika na jamii jinsi inavyotoa ushawishi kuhusu jinsi
tunavyowathimini watu. Harakati ya wanawake inaweza kushughulikia maswala haya muhimu
sana, ili pia tunahitaji vuguvugu la taratibu za vyombo vya dola kudhibitiana ili kuzuia matumizi
mabaya ya madaraka linaloongozwa na wanaume.
Jambo hili linafaa kuwa hatua ya kusonga mbele; mwisho wa kutojali na mateso ya kimya kimya
ya wanawake katika maeneo ya vijijini na mijini, pamoja na wanawake wanaofanya kazi
majumbani. Wanaharakati wa leo wanatakiwa kuwawezesha wale wanaoelekea kuachwa
nyuma, wengi wao wakiwa wanawake, kutokana na maelezo ya ripoti yetu ya hivi karibuni,
Kufanya Ahadi Zetu Kivitendo yaani Turning Promises into Action. Katika kanda zote, wanawake
wanaelekea kuishi katika ufukara kuliko wanaume. Pengo hili la kijinsia ni kubwa na kufikia
asilimia 22 ya kundi la watu wenye rika ya umri kati ya miaka 25 – 34—umri muafaka wa uzazi
kwa wanawake, huku ikionekana wazi wazi wanawake hawa wakiishi kwa shida sana na kukosa
huduma muhimu—kutokana na hali hii kunahitajika marekebisho ya sera na hatua muhimu.
Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshughulikia Maswala ya Wanawake lina mahusiano
maaalumu na vuguvugu la Wanawake; chimbuko letu ni uharakati. Asasi za Kiraia kihistoria zina
jukumu muhimu katika kuongoza hatua ya kiulimwengu kuhusu usawa wa kijinsia kwa
kuhamasisha marekebisho, kwa kuweka mkazo juu ya hali tete ya changamoto za wanawake,
kutoa ushawishi dhidi ya sera, kwa kushiriki katika ufuatiliaji, na kusisitiza uwajibikaji.
Tunapaswa kwa makusudi kubuni mpango kabambe wa kuunga mkono harakati ya kisiasa ya
wanawake na kutenga eneo pana zaidi kwa ajili ya kusikika kwa sauti hatua za Asasi za Kiraia za
Wanawake ili kuunganisha juhudi zetu na zile za watu wanaohitaji haswa kuleta mabadiliko
zaidi. Utamaduni wa umasikini uliojikita katika jinsia, ukatili na unyonyaji unatakiwa
kukomeshwa na kizazi kipya na kuletwa na usawa wa kudumu.
***

This entry was posted in Uncategorized on by .

About STELLA VUZO

UNIC Dar es Salaam is pleased to be of service to the people of Tanzania, providing prompt and accurate information on the work of the United Nations. Please share your views and comments. You can also engage our discussions on unicdaressalaam facebook page and follow us on twitter@UNICDaressalaam.